NYOTA WA TAARAB "MARIAM HAMIS' 'PAKA MAPEPE' KUZIKWA LEO.
![]() |
| Baadhi ya waombolezaji walifika nyumbani kwa marehemu. |
MWIMBAJI mahiri wa taarab nchini Mariam Hamis ambaye
amefariki jana alfajiri katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matatizo ya uzazi, atazikwa leo saa kumi jioni katika makaburi
ya Magomeni Fundikira.
Mariamu ambaye alitamba na wimbo wa Paka Mapepe ambao
aliuimba akiwa katika bendi ya East African Melody mpaka umauti unamkuta,
alikuwa mwanamuziki wa bendi ya TOT taarab ambayo alijiunga mwaka juzi akitokea
katika bendi ya Five Stars.
Chanzo:Global Publishers

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA