MASTAA WA KIKE WATIA DOA KISOMO CHA STEVE NYERERE.
BAADHI ya mastaa wa kike Bongo wakiwemo Irene
Uwoya, Sauda Mwilima, Salma Salmin ‘Sandra’ na Zuena Mohammed ‘Shilole’
wamekitia doa kisomo kilichoandaliwa na msanii mwenzao, Steven Mangere
‘Nyerere’ kufuatia kwenda kinyume na taratibu za dini ya Kiislam.
Steven Mengele ‘Steve Nyerere’ aliyeandaa kisomo hicho.
Akizungumza na safu hii, ustadhi Juma Salum wa madrasa ya
Kinondoni jijini Dar alisema, alichokifanya Steve Nyerere ni kitu kizuri ila
kuna baadhi ya mastaa wa kike wameitia doa shughuli hiyo kwa kutofunika vichwa
vyao.
“Kwenye Uislam mwanamke kuacha nywele zake wazi ni kosa,
nimeshangaa kuona baadhi ya mastaa kwenye ile shughuli ya Steve wakiwa vichwa
wazi na walikuwa ‘bize’ kuomba dua, kimsingi dua zao ni vigumu sana
kupokelewa,” alisema ustadhi huyo.Hivi karibuni Steve Nyerere aliandaa kisomo
na kuwaita maustadhi pamoja na wasanii wengine lengo likiwa ni kuwaombea mastaa
waliotangulia mbele ya haki pamoja na kuondoa mikosi na balaa kwenye tasnia ya
filamu Bongo.


No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA