MATOKEO CCM: RAIS KIKWETE ACHAGULIWA TENA KUWA MWENYEKITI, MANGULA NA SHEIN MAKAMU MWENYEKITI.
Mwenyekiti wa CCM, Taifa, Jakaya Kikwete na Makamu wake
wawili Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein (Zanzibar) na Philip Mangula
(Bara) wakiwa meza kuu baada ya kutangazwa kushika nyandhifa zao.
Matokeo ya nafasi za makamu mwenyekiti Zanzibar na Tanzania Bara yametangazwa rasmi,
ambapo hakuna kura iliyoharibika hivyo wamepita kwa asilimia 100%.
Dr. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar amepita kwa idadi ya
kura 2397 na hakukuwa na kura za hapana, hivyo kutangazwa rasmi kuwa ndio
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, wakati huo huo Philip Mangula amechaguliwa
kwa kura 2397, hakuna zilizoharibika hivyo Mh. Mangula ndio Makamu Mwenyekiti
mpya kwa upande wa Tanzania Bara.
Wajumbe wakiserebuka baada ya Rais Jakaya Kikwete kutangazwa
kuwa mshindi wa Uenyekiti wa CCM, Taifa.


No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA