'NAY WA MITEGO' AMKANA 'NISHA', ADAI HAYUPO KWENYE MAHUSIANO NA MWANAMKE YEYOTE.
WAKATI watanzania wengi wakiamini kuwa msanii Ney Wa Mitego,
yupo kwenye mahusiano ya kimapenzi na mwanadada wa kwenye tasnia ya filamu
Salma Jabu ’Nisha’, mkali huyo wa ngoma ya ‘Wamenichokoza’, amekanusha uwepo
wake kwenye mahusiano na mwanamke yeyote na kudai kuwa kwa sasa ana marafiki tu
wa kike wa kubadilishana mawazo na si wapenzi au mpenzi kama watu wanavyodai.
Hata hivyo kauli ya msanii huyo inaweza kuzua utata mkubwa
kwani mashabiki wake wengi wanajua kuwa mpenzi wake ni mwanadada huyo wa bongo
movie ingawa tangu kutoka kwa habari hizo hakuwahi kuzungumza lolote juu ya
mahusiano hayo kama ni kweli.
“Hapana kwa sasa sina mpenzi, nimeshatoka na wanawake kadhaa
hilo lipo wazi
lakini kwa sasa natafuta yule mpenzi mwenye tabia njema,” alisema.

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA