MSANII LORD EYES: WAKILI WAKE ATOA UFAFANUZI KWA WAANDISHI WA HABARI KUFUATIWA TUHUMA ZINAZOMKABILI LORD EYEZ.
|
Msanii Lord Eyes na mwanasheria wake Peter Kibatala wakiwa
Double View ambapo walizungumza na waandishi wa habari.
|
|
Msemaji wa kundi la WEUSI Nikki wa Pili,Mwanasheria,Lord
Eyes na G Warawara.
|
Wakili wa Lord Eyes leo ametoa ufanunuzi kuhusu tukio
lililotokea la msanii huyo kuhusishwa na wizi wa vifaa vya kwenye gari.Wakili
huyo alisema kua dhumuni la kuwaita waandishi wa habari leo ni kutaka Jamii
itoe nafasi kwa vyombo vya sheria kutoa majibu juu ya tuhuma hizo baada ya hapo
ndo waanze kuongea.
Sahivi kinachoendelea ni habari ambazo watu hawana uhakika
nazo.Wakili huyo alisema kuwa Lord Eyes hana hatia hadi pale vyombo vya sheria
vitakaposema kuwa msanii huyo kweli anahusika na shutuma hizo za uwizi.Kwa
upande wa Lord Eyes amesema kuwa watu wanajua kuwa yeye ni mwanamuziki kwa muda
wote na hajihusishi na maswala ya uwizi na ameomba mashabiki wavumilie kipindi
hichi ambacho anapigania haki na ukweli utajulikana.
Wakili wa msanii Lord Eyes Peter Kibatala akieleza tukio zima la msanii Lord Eyes...MSIKILIZE akizungumzia tukio zima la msanii huyo na dhumuni la kuitisha mkutano na waandishi wa habari.
|
| NICK WAPILI AKIWA ANAFUNGUKA. |
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA