Header Ads

Breaking News
recent

MAMA KANUMBA NA SETH, VILIO VINAENDELEA.


Mama Mzazi wa Steven Kanumba, Flora Mtegoa akilia juu ya kaburi la mwanae.
 MIEZI saba tangu msanii maarufu wa filamu Bongo, Steven Kanumba kuiaga dunia Aprili 7, 2012 bado majonzi na vilio vimeendelea kuitikisa familia yake ambapo hivi karibuni mama yake, Flora Mtegoa na mdogo wake, Seth Bosco waliangua vilio upya juu ya kaburi lake.

Mama Kanumba na Seth wakilifanyia usafi kaburi la Kanumba.
.“Mimi sitaacha kumlilia mwanangu Kanumba jamani na siwezi kumsahau maana kifo chake kilikuwa cha ghafla sana wakati tulikuwa tumepanga mambo mengi.
“Nina muda sijaja kuliona kaburi lake, tangu lilivyojengwa upya sijafika ndiyo leo nakuja huku kwa ajili ya kuliona na kulifanyia usafi. Maskini mwanangu, lala kwa amani baba,” alisema mama huyo huku akilia kwa uchungu ambapo Seth naye alishindwa kujizuia.
Na Gladness Mallya
 Huu ndio ujumbe ulioandikwa katika kaburi la Steven Kanumba.

 Mdogo wake Marehemu Kanumba, Seth Bosco akiweka shada la maua katika kaburi la kaka yake.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.