JOKATE AIBIWA IPAD UKUMBINI.
ALIYEKUWA mshehereshaji katika Shindano la Miss
Tanzania 2012, Jokate Mwegelo juzikati alijikuta akilizwa iPad yake ndani ya
Ukumbi wa Cristal Palace uliopo kwenye Hotel ya Blue Pearl, Ubungo Plaza,
jijini Dar.
![]() |
Tukio hilo lilijiri wakati warembo waliokuwa wakishiriki
shindano hilo wakifanya ‘riheso’ ambapo Jokate aliiacha iPad yake na kwenda
kufanya majaribio ya kipaza sauti alichotakiwa kukitumia.
“Jamani iPad yangu ilikuwa hapa mbona siioni, naomba
aliyeichukua anirudishie, nataka kuondoka kwenda kujiandaa,” alisikika Jokate.
Baada ya kupita takriban nusu saa bila majibu, ndipo
uvumilivu ulianza kumshinda mlimbwende huyo na kuanza kutokwa machozi baada ya
kuona dalili za kurudishiwa hazikuwepo.
Mpaka Amani linatoka ukumbini hapo saa nane mchana, mrembo
huyo hakufanikiwa kuiona iPad yake ambayo inakadiriwa kuuzwa kwa shilingi
milioni moja za Kibongo.
Stori: Shakoor Jongo


No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA