DIAMOND APATA BALAA... NI AJALI MBAYA YA GARI.
![]() |
MWANAMUZIKI wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul Juma ‘Diamond’, amepatwa na kile kinachoonekana ni balaa nambari moja tangu apate umaarufu.
![]() |
|
Gari la Diamond aina ya Toyota Land Cruiser Prado TX baada
ya kugongana na Toyota Rav 4.
|
![]() |
Jumamosi iliyopita, Diamond akiwa anaendesha gari lake la kifahari
aina ya Toyota Land Cruiser Prado TX, aligongana na Toyota Rav4, lililokuwa
linaendeshwa na mwanamke mmoja ambaye jina lake halijapatikana.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Charles
Kenyela, Diamond aligongana na mwanamke huyo kwenye Barabara ya Kimweri,
Msasani, Dar es Salaam, saa 3 usiku.
Kenyela alisema, askari wa barabarani walichunguza na
kubaini kuwa chanzo cha ajali hiyo ni pikipiki ambapo wakati Diamond anakata
kona, alijaribu kuikwepa pikipiki hiyo ndipo akakutana uso kwa uso na Rav4 la
mwanamke huyo.“Baada ya kugongana, gari la Diamond liliendelea kuserereka na
kuigonga pikipiki pamoja na aliyekuwa anaiendesha. Hakuna aliyefariki kwenye
ajali hiyo, wote walipata maumivu.”
Kwa upande mwingine, ilibainika kuwa Diamond baada ya kupata
ajali hiyo, alikwenda Hospitali ya TMJ kwa matibabu baada ya kujihisi amepatwa
na maumivu.
Diamond hakupatikana ili kuzungumzia ajali hiyo lakini kwa
kumbukumbu, kabla ya kumiliki gari hilo la kifahari aliwahi kumiliki magari
mengine mawili, likiwemo lile alilokaa nalo kwa muda mrefu, Toyota Opa lakini
hakuwahi kupata ajali ya kiwango hicho.
Na Makongoro Oging'



No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA