CHAMA CHA MAKAHABA CHASAJILIWA RASMI.
Rais wa Malawi Joyce Banda.
ZAIDI ya makahaba 2000 nchini Malawi wameungana kwa ajili ya
kupinga manyanyaso wanayoyapata na kuboresha mazingira ya afya, baada ya
kuzindua rasmi chama cha kuwatetea juzi.
Kundi hilo linaundwa na vyama visivyo vya kiserikali vya
ndani na nje ya nchi hiyo, ikiwa ni la kwanza kutambuliwa rasmi na kupewa
usajili katika nchi hiyo ya kusini mwa Afrika ambapo biashara ya ukahaba
inaharamishwa.
“Muda wa kujadili kwa pamoja matatizo yanayowakabili ndio
huu. Mnajua namna Polisi na Mahakama vinavyowabana na kwamba mnahitaji kupata
huduma nzuri za kulinda afya zenu na afya ya uzazi bila kipingamizi,” alisema
mwanasheria wa haki za binadamu, Chrispin Sibande alipokuwa akizungumza na kundi
la wateja wake wapatao 50 ambao ni makahaba.
Makahaba nchini humo mara nyingi wamekuwa wakikamatwa na
Polisi hata kwa makosa madogo ikiwemo kukutwa wakiwa wamekaa bila kazi, ambayo
pia huambatana na kutozwa faini.
Miaka mitatu iliyopita, makahaba 14 walikamatwa na Polisi na
kulazimishw akupimwa Virusi vua Ukimwi (VVU) na wote kukutwa wakiwa
wameathirika, ambapo walishtakiwa mahakamani kwa kufanya biashara ya ngono huku
wakijua kuwa wana maradhi hayo ya kuambikiza, ambapo walichajiwa Dola7 kila
mmoja na kuachiwa huru.
Baadaye waliishtaki Serikali ya nchi hiyo kwa kuingilia
mambo yao binafsi katika kesi ambayo hadi sasa bado inasubiri kusikilizwa
katika mahakama kuu.
Wataalamu wa afya nchini humo wanasema maambukizi ya Ukimwi
miongoni mwa makahaba hao yanafikia asilimia 70. Mawakili wao wanasema kuw
awanatumiani umoja wao utawasaidia pia katika kuwaelimisha kuepuka maambukizi
hayo.
Habari na Mwananchi.

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA