WOLPER ASEMA ATABAKI KUWA MUISLAM MILELE NA MILELE.
Asili Yetu Tanzania.Copyright
MSANII wa filamu ambaye alisilimu, Jacqueline Wolper amesema
licha ya kwamba ameachana na mchumba wake Ramadhani Mtoro ‘Dallas’ atabaki kuwa
Muislam hadi mwisho wa maisha yake.
Wolper ambaye sasa anafahamika kwa jina la Ilham alisema, ni
kweli alibadili dini baada ya kuchumbiwa na Dallas lakini atakuwa anamchezea
Mungu kama ataamua kurudi kwenye Ukristo baada ya uchumba kuvunjika.
“Mimi nitabaki kuwa Muislam hadi kifo, siwezi kurudi kwenye
Ukristo kwani nilikuwa nikiupenda Uislam.
Akitokea mwanaume Muislam akataka kunioa niko tayari na hata
akija Mkristo pia ila nitaendelea kuwa Muislam,” alisema Wolper.
Wolper alibadili dini siku chache zilizopita baada ya
kuingia kwenye uhusiano na Dallas lakini hivi karibuni kulikuwa na madai kwamba
amerudi kwenye Ukristo, jambo ambalo amelikanusha.

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA