MAKEKE AFRIKA KOLEKSHENI INAKULETEA MITINDO NA UBUNIFU MPYA TANZANIA.
Asili Yetu Tanzania.Copyright
![]() |
KIOTA KIPYA CHA MASWALA YA UBUNIFU NA MTINDO
Mdau leo naomba kukutambulisha kwako kijana wa Kitanzania
anaekuja kwa kasi katika fani ya Ubunifu na Mitindo, Kwa majina anaitwa JOCKTAN
MALULI akiwa chini ya Kiota Chake cha MAKEKE AFRIKA KOLEKSHENI ambapo ameamua
kuleta mapinduzi makubwa katika kilinge cha Mitindo na Ubunifu hapa Tanzania lakini pia nje ya Mipaka ya Tanzania.
Inawezekana kabisa jina la kijana na kazi za kijana huyu
mwenye MAKEKE mengi zikawa hazijulikani sana,
JOCKTAN MALULI maarufu kwa jina la MAKEKE ni mhitimu wa shahada ya Sanaa ya
Uchoraji na Ubunifu katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
Akiamini kabisa kwamba soko la sanaa ya Ubunifu na Mitndo
likiwa na Ushindani mkubwa hapa nchi MAKEKE anajivunia uwezo wake mkubwa katika
fani hii akitumia mbinu mbalimbali zilizo kichwani mwake kwani si tu kipaji
pekee alichonacho bali MAKEKE ana elimu ya sanaa hii ya Mitindo.
Mpaka sasa MAKEKE AFRIKA KOLEKSHENI imeshashiriki katika
Matamasha mbalimbali ya Ubunifu na Urembo ikiwa pamoja na Redds Fashion Mbeya,
Redds Fashion Dodoma, Dom Fashion Night, na UDOM Fashion Soul.
Kijana huyu ameshafanya kazi pamoja na Magwiji wa sanaa hii
ya Ubunifu na Mitindo hapa nchini kama AILINDA SAWE, kwa sasa MAKEKE anafanya
kazi na gwiji mwengine Mustafa Hassanali akiwa ni Graphics Designer. Kwa
taarifa zake nyingi Faceboo: MAKEKE AFRIKA KOLEKSHENI; Simu : +255754411889
BAADHI YA KAZI ZA MAKEKE AFRIKA KOLEKSHENI
![]() |
![]() |



No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA