REDD'S MISS TALENT KUPATIKANA LEO.
Asili Yetu Tanzania.Copyright
| Warembo wakiwa katika moja ya mitoko. |
Mshindi wa taji hilo atafanikiwa kuingia hatua ya 15 Bora ya
Redd’s Miss Tanzania, hivyo kuungana na washirii wengine wawili ambao
wamefanikiwa kukata tiketi hiyo.
Warembo ambao mpaka sasa wamejihakikishia kuingia hatua hiyo
ni Lucy Stephano, aliyetwaa taji la Miss Photogenic, Magdalena Roy
anayeshikilia lile la Top Model na Mary Chizi aliyetwaa lile la Redd's Miss
Tanzania Sports Lady.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam
jana, Afisa Habari wa Redd’s Miss Tanzania, Haidan Ricco alisema kila kitu
kimekamilika na kinachosubiriwa ni kujua nani ataibuka na ushindi.
“Kutakuwa na burudani kadhaa ambazo zitatolewa na wasanii maarufu
hapa nchini, huku washiriki hao wa Redd’s Miss Tanzania nao watatoa burudani za
kufa mtu kwa mashabiki.”
Ricco alisema katika shindano hilo linalotarajiwa kuanza saa
2 usiku, huku kiingilio kikiwa ni Sh 10,000.
Shindano la Redd’s Miss Tanzania kwa sasa linadhaminiwa na
kinywaji cha Redd’s Original kinachozalishwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA