Header Ads

Breaking News
recent

RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE AKIWA KATIKA ZIARA NCHINI CANADA.

Asili Yetu © All rights reserved


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongozana na  Gavana Jenerali wa Canada Mhe. David Johnson na mkewe Mama Sharon Johnson kuingia  jumba la Rideau jijini Ottawa, Canada, katika hatua yake ya kwanza ya  ziara rasmi ya siku mbili jijini humo Jumatano Oktoba 4, 2012.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika viwanja vya jumba la Rideau Hall jijini Ottawa, Canada, katika hatua yake ya kwanza ya  kuanza ziara rasmi ya siku mbili jijini  humo Jumatano Oktoba 3, 2012. Jumba hilo ndilo makazi  na ofisi rasmi ya Gavana Jenerali wa Canada tangia mwaka 1867 ambapo pamoja na kuishi humo pia hapo ndipo hutumika kwa kuwatunukia wananchi wa Canada waliofanya vyema, pa kupokelea wageni mashuhuri wa nchi za nje na pia ndipo anapofanyia shughuli zote za kitaifa akiwa kama mwakilishi wa Malkia wa Uingereza.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride rasmi katika viwanja vya jumba la Rideau Hall jijini Ottawa, Canada, katika hatua yake ya kwanza ya  ziara rasmi ya siku mbili jijini  humo Jumatano Oktoba 3, 2012. Jumba hilo ndilo makazi  na ofisi rasmi ya Gavana Jenerali wa Canada tangia mwaka 1867 ambapo pamoja na kuishi humo pia hapo ndipo hutumika kwa kuwatunukia wananchi wa Canada waliofanya vyema, pa kupokelea wageni mashuhuri wa nchi za nje na pia ndipo anapofanyia shughuli zote za kitaifa akiwa kama mwakilishi wa Malkia wa Uingereza.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.