Header Ads

Breaking News
recent

HOTEL YA KIFAHARI KWAAJILI YA MBWA YAFUNGULI NEW YORK MAREKANI, HUDUMA SAWA NA ZA BINADAMU..


Hii ndio hotel ya kifahari ya mbwa iliyoko jijini New York Marekani.
Leo ni siku ya wanyama duniani, pengine wewe na mimi tulikuwa hatujui kuwa Mbwa wanahotel zao maalumu ambapo hupelekwa kupumzika na kupewa starehe mbali mbali. Mbwa mmoja kwa siku analipiwa kiasi cha dola 200 kutoka kwa mwenye Mbwa.

Hotel ya kwanza kuanzishwa kwaajili ya Mbwa  huko Marekani sehemu za Hollywood ilianzishwa miaka minne iliyopita kwa lengo la wakati mwenye Mbwa anapokwenda likizo ya mapumziko katika hotel za kifahari, basi na Mbwa wao nae apelekwe kwenye hotel  itakayo mpatia raha, kama mazoezi, chakula kipya na mafunzo mbali mbali, Shawn "Hassanzadeh" mmiliki wa hotel alisema.

Moja ya huduma katika vyumba vya Mbwa hawa ni kuwekewa TV na huduma nyingine sawa na binadamu.

Mbwa wakiwa meazani - kama vile wanakikao.
Mmoja wa wahudumu akimpatia mafunzo mbwa.
Hii ni sehemu ya mbwa kupumzika.
 Mbwa akifundishwa.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.