SEMINA NA MAONYESHO YA "TWENDE" NI KUANZIA TAREHE 8 HADI 20 MWEZI HUU KATIKA VIWANJA VYA MNAZI MMOJA JIJINI DAR ES SALAAM.
|
Washiriki wa TWENDE 2011, wakisalimiana
na Waziri wa Viwanda na Biashara Dr. Cyril Chami mara baada ya waziri huyo
kuwatembelea katika banda lao na
kujionea bidhaa wanazotengeneza.
|
|
Washiriki wa Jukwaa la Wanawake Wajasiriamali Tanzania- TWENDE,
2011,
kutoka mikoa tofauti ya Tanzania na nje ya nchi wakionyesha bidhaa zao katika
viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam.
|
SEMINA NA MAONESHO YA TWENDE NI KUANZIA TAREHE 18 HADI 20 YA
MWEZI WA KUMI KATIKA VIWANJA VYA MNAZI MMOJA JIJINI DAR ES SALAAM.
WANAWAKE WAJASIRIAMALI KUELIMIKA, KUUZA BIDHAA ZAO NA KUKUZA
MTANDAO WA KIBIASHARA KUPITIA JUKWAA LA WANAWAKE WAJASIRIAMALI TANZANIA- TWENDE
Jukwaa la Wanawake Wajasiriamali Tanzania- TWENDE
linatarajia kufanyika kuanzia tarehe 18 – 20 ya mwezi wa kumi 2012 katika
viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
TWENDE imekuwa ikifanyika kila mwaka kwa mwaka watatu sasa
tangu kuanzishwa kwake mwaka 2010, lengo likiwa ni kuwaleta pamoja wanawake
wajasiriamali wadogo, wakubwa na wale wanaochipukia ili kupata fursa ya kuuza,
kuonesha na kujadili masuala ya biashara kwa ujumla.
Sambamba na hilo. TWENDE inalenga kusaidiana na serikali
katika kutimiza malengo ya milenia likiwemo lengo namba moja ambalo linalenga
kuondoa umasikini, namba tatu kutetea haki na fursa sawa kwa wanawake, lengo
namba tano kuhamasisha afya ya uzazi na
lengo namba nane, ambayo ni kuendeleza uhusiano wa kudumu kwa ajili ya maendeleo
ya jamii. Pia TWENDE inalenga Kukuza uzalishaji kwa wanawake wafanyabiashara na
kukuza mgawanyiko wa masoko sambamba na muonekano wa wafanyabiashara wanawake
katika jamii.
Kwa upande wa mwaka huu TWENDE inatarajia kuwashirikisha
wanawake wajasiriamali wengi zaidi ambao wamekuwa wakifanya biashasha tofauti
ili kuweza kupata fursa ya kubadilishana uzoefu na kuongeza ujuzi zaidi
kibiashara. Sambamba na semina bora zitakazotolewa kwa wanawake wote ambao
watapata elimu itakayotolewa wataalamu wa fani mbalimbali
Kwa miaka mitatu mfululizo TWENDE imekuwa ikitoa fursa kwa
wanawake wajasiriamali kukutana pamoja na kujadili mafanikio na changamoto
ambazo zimekuwa ni kikwazo cha wanawake wajasiriamali kutofikia malengo yao
kibiashara.
“Licha ya kwamba wanawake wengi wamejikita katika sekta hii
ya ujasiriamali, lakini bado wamekuwa wakikabiliawa na changamoto mbalimbali
zinazokwamisha kufikia malengo yao, ikiwemo elimu ya ujasiriamli na upatikanaji
wa mikopo, kwa hiyo ipo haja kwa wanawake kujijengea utaratibu wa kushiriki
katika fursa kama hizi zinazowajengea uwezo”. Alisema Saphia Ngalapi Meneja
Mradi wa TWENDE.
Zaidi ya Wanawake Wajasiriamali Wanawake 100 kutoka mikoa
mbalimbali ya Tanzania Bara na Tanzania Visiwani wanatarajai kushiriki katika
TWENDE mwaka huu, ampabo maonesho hayo yanakwenda sambamba na semina zitakazo
tolewa kwa wanawake wote bure, kwa wale watakaoshiriki katika maonesho, na hata
wale ambo watakuwa hawakupata frusa ya kuonesha na kuuza bidhaa zao.
KUHUSU TWENDE
Tanzania Women Entrepreneurs & Networking Development
Exposition (TWENDE) inapanga kuleta maendeleo kwa wanawake wajasiriamali kwa
kuandaa jukwaa ambalo litakua mahususi kuweza kukutana zaidi ya wanawake
wafanyabiashara 100 wadogo, wakati na wakubwa kutoka viwanda vikubwa na vidogo,
taasisi za serikali na mashirika yasio ya kiserikali (NGO).
Tanzania Women Entrepreneurs & Networking Development
Exposition (TWENDE) pia inalenga kuyapa fursa makampuni kukutana yakikidhi
malengo ya wahudhuriaji. Ni sehemu ya kuuza na kuonyesha bidhaa na huduma za
kampuni mbalimbali kwa wafanya maamuzi. Maonyesho haya yataenda sambamba na
mkutano wa siku tatu utakaotoa elimu bora kwa washiriki. Kwa habari zaidi
tembelea www.twende.info
MTAZAMO WA TWENDE
Ni kuwaelimisha kuwahamasisha na kuwaendeleza wanawake
Tanzania. Twende
CONTACT: Davis Mwijage
:+255
712 847881
davis@361tanzania.com
--
Hassan Mrope
PR TWENDE EVENT 2012
361 DEGREES
PR | EVENTS | MEDIA | Company
P.O.Box 10684, 105 Kilimani Road,
(Next to Embassy of France/Near NIDA Offices)
Kinondoni, Dar es Salaam, Tanzania.
Tel : +255 (0)22 266 8555
Mobile : +255 (0)713 441 892
Social Media : www.twitter.com/361tanzania
www.facebook.com/361TANZANIA
Web : www.361tanzania.com
www.twende.info

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA