Header Ads

Breaking News
recent

PICHA ZA MAANDAMANO YA WAISLAMU MBAGALA - WAHARIBU BAADHI YA MAKANISA.

Asili Yetu Tanzania.Copyright

Gari la Clouds Media likiwa limeharibiwa vioo na waandamanaji wa kiislamu Mbagala jijini Dar es salaam.
Baadhi ya waandamanaji.

Askari wa kutuliza ghasia wakipambana na waandamanaji.
Gari la kumwaga maji ya machozi, likifanya kazi yake kwa aandamanaji.

Askari wakivuka mtaro pamoja na waandamanaji waliotiwa nguvuni.
Barabara ikiwa imezibwa kwa moto na waandamanaji.
  


Baadhi ya waandamanaji wakiwa chini ya ulinzi.
HAMISI SALUM BABA

VURUGU kubwa zilizuka baada ya mtoto Emanuel Josephat(14)’ kukojolea kitabu cha Quraan cha dini ya kiislam, swala hili liliingia katika hatua nyingine baada ya waumini wa dini ya kiisilam kukusanyika wakishinikiza kuachiwa kwa mtoto huyo ili wamuue.

Waumini hao wanaokadiriwa kufikia idadi ya 3000 baada ya kutawanywa na Polisi waliingia mitaani na kuchoma kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT), Mbagala Zakhem, Kuharibu Kanisa la Anglican,kuvunja vioo katika kanisa la Wasabato, huku kanisa la Tanzania Assembly of God(TAG), Mbagala Kizuiani wakilichoma moto na kuchukua vifaa vya muziki na kuviunguza hadharani.

Vurugu hizo zilizotokea jana jijini Dar es Salaam, majira ya saa 5 asubuhi ambapo waislamu hao walivamia kituo cha polisi Maturubai,Mbagala Kizuiani.

Vurugu hizo ambazo zimesababisha gari za polisi namba T142 AVV,PT 0966 na T 325 BQP,basi la uda na gari la waandishi wa habari kutoka Clouds zikiharibiwa kwa mawe na waandamanaji hao.

Awali waamini hao walikusanyika katika kituo hicho cha polisi wakimtaka mtoto huyo ambaye alikuwa chini ya ulinzi aachiwe na Polisi walipogoma kufanya hivyo ndipo vurugu hizo zilipoanza.

Kikosi cha kutuliza ghasia kilionekana kuzidiwa nguvu na watu hao ambao walikuwa wakiwatawanya kutoka eneo moja wanakimbilia eneo lingine na kuleta madhara mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufunga barabara.

Hatahivyo baada ya viongozi wa dini hiyo kufika wakiwa wameambatana na Sheikh wa Wilaya ya Temeke, Sheikh wa Taasisi na Jumuiya za Waislamu kukaa kikao na kamanda wa Polisi Wilaya ya Temeke, David Misime, walifikia muafaka wa kuwaita waislamu hao na kuwatuliza lakini hali iliendelea kuwa si shwari kwani baada ya viongozi hao kuona waandamanaji hao wakikamatwa na kupigwa walikuja juu na kutishia kuondoka.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.