KABURI LA KANUMBA LAJENGWA UPYA - Familia yake yazungumza jambo..
Asili Yetu Tanzania.Copyright
![]() |
KABURI la aliyekuwa msanii maarufu wa filamu Bongo, Steven
Kanumba limeanza kujengwa upya ikiwa ni siku chache baada ya wasanii wenzake
kushushuliwa kuhusiana na muonekano wake ulivyokuwa.
Hatua ya kulijenga upya kaburi hilo imechukuliwa na Mama
yake mzazi, Flora Mtegoa na kampuni ya Steps kutokana na mauzo ya kazi zake mbalimbali za filamu, hivyo wameona ni vyema wakalijenga upya kwani
lilikuwa ni gumzo kwa watu mbalimbali waliokuwa wakihoji hadhi ya kaburi hilo
na umaarufu wa marehemu Kanumba.
Akizungumza na paparazi wetu, Mama Kanumba alisema kauli za
kaburi hilo kujengwa upya zilikuwa kama
wimbo wa taifa lakini kuna mambo alikuwa akiyamalizia, hivyo kwa
sasa ameshalijenga vizuri tofauti na lilivyokuwa mwanzo.
“Kaburi la Kanumba tumelijenga upya japokuwa baba yake
alisema hakuna haja ya kulijenga tena lakini mimi ndiyo nina uchungu na
mwanangu japokuwa ameniacha bado nampenda na nitaendelea kumkumbuka, kwa
kushirikiana na kampuni ya Steps tumelijengea vizuri,” alisema Mama Kanumba.
Hivi karibuni wasanii mbalimbali wa filamu Bongo
walilitembelea kaburi hilo na kupatwa na uchungu lakini walishushuliwa na
mwenzao na kwa kuwaambia kuwa wamelisusa kaburi hilo.
Alisema hadhi na umaarufu aliokuwa nao Kanumba hakustahili kulala kwenye kaburi lile, hivyo aliwataka
kuchangishana fedha ili walijenge vizuri lakini hakuna aliyemuunga mkono badala
yake waliishia kupeana maneno mbofumbofu.
Chanzo: Global Publishers

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA