CHRISTIANO LONALDO, ANUNUA GARI MPYA YENYE THAMANI YA SH. 415 MILIONI - YENYE SPEED YA 100 KWA SAA.
Asili Yetu Tanzania.Copyright
![]() |
NYOTA wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amejawa na furaha
tele kutokana na kiwango cha juu alichoanza nacho msimu huu na kuamua
kujipongeza kwa kujinunulia gari dogo jipya la kifahari kwa ajili ya kutanulia
mitaani.
Gazeti la Marca limeandika leo kuwa Ronaldo amenunua gari
hilo jipya aina ya McLaren MP4-12C Spyder kwa dola za Marekani 268,000 (Sh.
milioni 415).Sifa mojawapo kubwa ya gari hilo la kisasa ni kasi yake ya
kuchanganya mwendo kwani linapowashwa tu, huwa na uwezo wa kufikia spidi ya
kilomita 100 kwa saa baada ya muda mfupi wa sekunde 3.1.
Ronaldo alionekana juzi katika maeneo ya kwao, Lisbon nchini
Ureno ambako amekwenda kuungana na wenzake katika kambi ya kikosi cha timu ya
taifa ya Ureno.
Mbali na gari hilo jipya (McLaren MP4-12C Spyder) Ronaldo
pia anamiliki magari kadhaa ya kifahari likiwamo aina ya Lamborghini Aventador
LP700-4.

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA