JOKATE AZINDUA KIDOTI, NI KAMPUNI YA MITINDO NA UREMBO.
Asili Yetu Tanzania.Copyright
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kidoti Jokate Mwegelo
akizungumza wakati alipozindua rasmi kampuni hiyo inayojishughulisha na Uuzaji
wa Nywele za Style mbalimbali Ubunifu wa
mavazi ambapo ameongeza kuwa nywele hizo zimejaribiwa na kukidhi matakwa ya kudumu,
kuweza kutumiwa tena na tena, uzito pamoja na msokotano na zitakuwa
zikipatikana katika mitindo na urefu mbalimbali zitazotumiwa na wasichana na
kinamama.
Ameongeza kuwa Nywele hizo pia zitawafikia watu wa mikoani
pia.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Kidoti Peter Kasiga pamoja na
CEO wa Kidoti Jokate Mwegelo wakijibu maswali kwa waandishi wa habari wakati wa
uzinduzi huo ambapo pia amefafanua kuzinduliwa rasmi kwa tovuti ya kampuni hiyo
leo itakayopatikana kupitia anuani ya www.kidotiloving.com
Kidoti ambayo ni chapa halisi ya Kitanzania imezinduliwa
rasmi leo jijini Dar es Salaam.
Chapa ya Kidoti imeundwa katika taswira yake mwenyewe
Jokate.
Sifa zake alizohakikisha zinaonekana kupitia Kidoti ni
pamoja na akili, ujasiri, dhamira, yenye kuthubutu lakini pia yenye bashasha
zote za kike.
Kidoti haitaishia katika mavazi na mitindo tu.
Kidoti ni harakati na mwanzo wa chapa ya mitindo-maisha
yenye nia kuu ya kuwezesha kizazi change,” aliongeza Jokate.
Nywele sanisi za Kidoti ambazo zimezinduliwa leo katika soko
ni zenye ubora wa hali ya juu zikiwa zimejaribiwa na wateja wake watarajiwa
wenyewe.
Mtiririko mzima wa ubunifu na uzalishaji wa bidhaa hizi
ulisimamiwa na kuongozwa na Jokate ambapo kila nywele zimejaribiwa na kukidhi
matakwa ya kudumu, kuweza kutumiwa tena na tena, uzito pamoja na msokotano.
Nywele hizi zinakuja katika mitindo na urefu mbalimbali
ambayo imebeba sifa za chapa hii zikiwa na mawimbo nyororo kwa ajili ya
wanawake wanaopenda kupendeza bila kufilisi mifuko yao.
Pamoja na ubora wake wa hali ya juu, nywele hizi zinaendana
kabisa na nia ya Kidoti ya kuvuruga na kuleta maana mpya katika tasnia ya
mitindo kwa ubunifu wa kuweza kutengeneza mitindo mingi kutumia nywele moja na
sifa hii inawasilishwa kwa soko walengwa kibunifu kupitia kasha za bidhaa hizi
ambazo zimesheheni picha za Jokate mwenyewe akionyesha mitindo mbalimbali kwa
ajili ya kila nywele. Sifa hii ya kipekee pia inawasilishwa kupitia maneno
“nywele moja staili kibao!” yaliyochapishwa katika kila kasha.
Nywele za Kidoti zitapatikana kwa bei nafuu kupitia mawakala
mbalimbali wa jumla na rejareja jijini kuanzia leo na zitauzwa kwa kati ya Sh.
9,500 na 12,000.
Mawakala hawa ni pamoja na maduka ya jumla na rejareja
Kariakoo, saluni mbalimbali jijini na mtandao wa mawakala mikoani utakaokuwa na
bidhaa zetu kuanzia wiki ijayo.
Nguo za Kidoti zitatambulishwa rasmi katika soko mwakani
(2013) zikifuatiwa na vifuasi vya urembo pamoja na vipodozi.
Harakati ya Kidoti inaendeshwa na timu ya vijana wabunifu
pamoja na kwamba shughuli za Kidoti zinaendeshwa kutoka Dar es Salaam, chapa
hii ni ya kiulimwengu zaidi.
Chapa ya Kidoti ilianzishwa mwaka 2011 na Bi. Jokate Mwegelo
ambaye ni mmoja wa watu mashuhuri nchini, kwa nia ya kubadilisha mtazamo mzima
wa tasnia ya mitindo. Chapa hii itasheheni bidhaa mbalimbali zikiwemo nywele za
sanisi ambazo zimezinduliwa leo pamoja na chapa. Bidhaa nyinginezo ni pamoja na
nguo, vifuasi vya urembo pamoja na vipodozi.
Kidoti ni chapa yenye uwezo wa kubadilisha jinsi
tunavyoichukulia tasnia ya mitindo hivi sasa.







No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA