ASILI YETU BLOG: AIRTEL TANZANIA YAZINDU MINARA INAYOTUMIA NGUVU YA NISHATI YA SOLA VIJIJINI.
Asili Yetu © All rights reserved
![]() |
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel inayoongoza kwa kutoa
huduma zenye wigo mpana zaidi imezindua minara yake inayotumia Umeme unao tumia nguvu za nishati ya Jua
katika kijiji cha kimande kata ya itunguru mkoani Iringa. Uzinduzi huo ni moja kati ya mikakati ya
Airtel kuhakikisha inaendeleza mipango yake ya kupanua upatikanaji wa mawasiliano
katika maeneo mbalimbali nchini kirahisi, kupunguza gharama za uendeshaji na
kuhamasisha utunzaji wa mazingira katika maeneo yenye minara yake nchini.
Akiongea wakati wa uzinduzi huo Mwenyekiti wa kijiji cha
Kimande kata ya Itunungu Tarafa ya Pawaga Iringa Vijijini Bw, Andason Mpululu
ameushukuuru uongozi wa Airtel kwa kuweza kukabili changamoto za mawasiliano
kijijini hapo na kuwa sehemu ya uboreshaji wa uendeshaji wa biashara mbalimbali
hasa za kilimo cha mpunga ambapo hapo awali upatikanaji wa soko ulikuwa mgumu
sana kutokana na kutokua na mawasiliano thabiti kama ilivyo sasa.
“Kwa kupitia Mtandao na huduma ya Airtel money huduma za
kifedha zimeboreshwa, zimekua karibu zaidi na kuwawezesha wafanyabiashara
kupokea malipo ya bidhaa zao kirahisi, kwa gharama nafuu na bila usumbufu
wowote. Nimatumaini yetu kuwa kwa kupitia umeme wa sola gharama za mawasiliano
ya simu za mkononi yataaendelea kupungua na kuboreshwa zaidi na kuleta tija kwa
wananchi hasa wenye kipato kidogo” alisema bwana Mpululu.
Naye mkazi wa kata ya Itunungu bwana Jumanne Zuberi alisema
“tunashukuru sana serikali kuwawezesha wawekezaji kuwekeza katika sekta ya
mawasiliano na hivyo kufikiwa na mtandao wa Airtel. Hapo zamani upatikanaji wa
mawasiliano ulikuwa ni changamoto kubwa hivyo kuwafanya wakazi wa kijiji hapa
kutembea umbali mrefu kupata mawasiliano. Tunashukuru kwa sasa huduma za simu
kijini hapa zimeweza kuboresha shughuli mbalimbali za kiuchumi, kijamii na
kuboresha usalama wa raia na mali zetu”.
Akiongea kwa niaba ya kampuni ya simu za mkononi ya Airtel
Meneja Uhusiano bw, Jackson Mmbando alisema” nia yetu ni kubadili matumizi ya
mafuta ya diesel na generator kuendesha mitambo yetu ya mawasiliano na kutumia
umeme wa nishati ya jua ambao utasaidia katika kutunza mazingira na kupunguza
gharama za uendeshaji ambazo zitatuwezasha kutoa huduma kwa ufanisi Zaidi na
kwa gharama nafuu ili kuwafikia watanzania wengi zaidi na kusogeza huduma
mbambali za kijamii karibu na wananchi zikiwemo huduma za Elimu, Afya na
Mawasiliano. Kazi kubwa kwa wananchi nikulinda huduma hizi na kuzitumia vizuri
kwa shughuli za maendeleo vijijini”.
Mawasiliano ndio chachu ya maendeleo hivyo tunaamini kwa
kutumia umeme wa jua hata gharama za uendeshaji zitapungua hivyo kuwezesha ktoa
huduma zenye viwango vya juu kwa gharama nafuu kwa watumiaji na wateja wa
Airtel nchini nzima aliongeza Mmbando”
Kampuni ya Airtel katika kurahisisha mawasiliano nchini
inaendelea kufunga mitambo ya umeme wa sola katika maeneo mbalimbali nchini
ikiwemo ya Tanga, Sumbawanga, Kigoma na mikoa mengine mingi. Mpaka sasa Airtel
imefanikiwa kufunga mitambo minne inayotumia nguvu za jua katika mkoa wa iringa
Iringa vijijini.Mpaka sasa Airtel inaongoza kwa kutoa huduma zenye wigo mpana
na ina vijiji na miji 50.


No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA