Header Ads

Breaking News
recent

PREZZO KUMUOA GOLDIE MSHIRIKI WA BBA KUTOKA NIGERIA.

Asili Yetu © All rights reserved

                                                             GOLDIE NA PREZZO

 Mshindi namba mbili wa Big Brother Afrika Prezzo kutoka kenya, amefunguka katika tovuti moja ya huko nchini Nigeria kuwa atamuoa mwanadada Goldie kutoka Nigeria endapo atasema "Yes I Do".

Prezzo mwenye umri wa miaka 32 kutoka Kenya, amefunguka kuwa hakusafiri hadi Nigeria kucheza: bali kueleza hisia zake kwa mwanamke mrembo asilia, aliyemfanya ang'are katika jumba la BBA 2012.

PREZZO aliyeomba msamaha kwa wanigeria wote kwa jinsi alivyokuwa akimtenda mwanadada 'GOLDIE', ametangaza hadharani nia ya kumuoa 'Goldie' kwasababu walikutana pia hadharani katika jumba la BBA.Ameongeza kuwa atafanya vyovyote vile ili kumfanya GOLDIE kuwa mke wake.

PREZZO alifunguka "sikuweza kueleza hisia zangu kwa mwanadada GOLDIE kwasababu ......... lakini sasa nakuja kupambana ili nipate tuzo ya ukweli na yenyethamani katika ushindi wangu".

                                                                        PREZO NA GOLDIE

                                                                      PREZZO

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.