Asili Yetu © All rights reserved
Katibu mkuu kutoka ofisi ya Rais mazingira "Sazi Salula" akizungumza na waandishi wa habari leo mjini Arusha kuhusu mkutano wa mazingira wa nchi za Afrika utakaofanyika Arusha.
Mawaziri barani Africa wanatarajia kufika mjini Arusha kuhudhulia mkutano mkubwa 14 wa mazingira utakao anza tarehe 10 hadi 14 mwezi wa tisa mwaka hu.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za mkoa mjini Arusha, mkurugenzi wa mazingira nchi za Afrika "Mounkaila Goumandakoye" ambaye ndiye mratibu wa mkutano huo, ameeleza kuwa mkutano huo wa mazingira utawahusisha mawaziri wa nchi za Afrika ambao watazungumzia mazingira na jinsi ya kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa inayoikabili Afrika kwa ujumla.
Naye katibu mkuu kutoka ofisi ya Rais mazingira "Sazi Salula" amefafanua kuwa Tanzania imepewa heshima kubwa katika kuandaa mkutano wa 14 wa mazingira ambapo waziri wa mazingira ndiye atakuwa mwenyekiti na mwenyeji wa mkutano huo unaotarajiwa kuanza mwezi ujao mwaka huu hapa mjini Arusha. Salula ameeleza kuwa Tanzania imepata nafasi pekee ya kuandaa mkutano huu kwa miaka miwili, yani 2012 na 213.
Hata hivyo mheshimiwa mkuu wa mkoa wa Arusha "Magessa Mulongo" alisema kuwa ni heshima kubwa nchi yetu Tanzania kuandaa mkutano mkubwa barani Afrika utakao kuwa na zaidi ya watu 3,000. Magessa amempongeza raisi wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuteuliwa mkoa wa Arusha kuandaa mkutano mkubwa wa nchi za Afrika. Pia mkutano huu utatanguliwa na mikutano mingine midogo kabla ya kuanza mkutano mkuu tarehe 10 hadi 14 mwezi septemba mwaka huu.
Mkuu wa mkoa ameongaza kuwa mkutano huu ni manufaa makubwa kwa wakazi wa Arusha kwani utanyanyua uchumi na kipato chao kupitia katika nyanja mbali mbali za kibiashara kama Hoteli, usafiri, huduma za kiafya na maeneo yote ya kibiashara mjini hapa.
Mkuu huyu amewaoomba wakazi wa mkoa wa Arusha na mikoa jirani kuwa watulivu na kuonyesha ukarimu kwa wageni watakao kuja katika mkutano huu, ili watakaporudi wapeleke sifa nzuri kwa nchi yetu.
Mkurugezi wa mazingira katika nchi za Afrika "Mounkaila Goumandakoye" ambaye ndiye mratibu wa mkutano huu wa mazingira akiongea na waandishi wa habari mjini Arusha.
Waandishi wa habari.


No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA