Asili Yetu © All rights reserve
Mama mmoja raia wa Thailand anakabiliwa na mashitaka ya mauwaji ya watoto wake wa kiume baada ya kuwachinja, kuwapika na kuwala, akidhania ni nguruwe.
Jarida moja kutoka Bangkok linaeleza kuwa polisi nchini humo ilipata ripoti hizo kuwa mama huyo (jina tunalihifadhi) jamii ya kabila la "Musur Hill" kaskazin mwa Thailand amechinja watoto wake wawili wenye umri wa kati ya mwaka mmoja na mitano na kuwapika na kula.Kwa mujibu wa jarida hilo, maafisa wa sheria walimkuta mwanamke huyo amelala na baadhi ya viungo vya mwili kiwa vimezagaa pembeni yake.
Mwanamke huyo aliripotiwa kuwa ni mgonjwa wa akili mnamo mwaka 2007, na hapo alikuwa nje ya matibabu kwa takribani miezi kadhaa hivi. Hatahivyo taarifa kutoka kwa wataalamu wa akili zimefunguka kuwa mama huyo mwenye ugonjwa wa akili siku ya tukio aliona kama watu wanamfata kumduru na hivyo tukio lilianzia hapo.
Hata hivyo kupitia vyombo mbali mbali vya habari vinaonyesha idadi ya matukio ya kula watu duniani yanaongezeka, huku mengine yakijihusisha na imani potofu za mila mbali mbali zikihusiana na kupata pesa za haraka haraka.

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA