Header Ads

Breaking News
recent

NEIL ARMSTRONG - MWANAANGA WA KWANZA KUFIKA MWEZINI AMEFARIKI DUNIA.

Asili Yetu © All rights reserved


Rais Obama alimuelezea Neil Armstrong kwamba ni mmoja kati ya mashujaa wakubwa wa Marekani, siyo wakati wake tu, lakini katika historia ya nchi hiyo piya.
Mwenzake Armstrong katika safari ya kihistoria ya kwenda mwezini mwaka wa 1969 alikuwa Buzz Aldrin, ambaye alisema Armstrong alikuwa rubani na kamanda mahiri.
Familia ya Neil Armstrong imetoa wito kwa Wamarekani kuonesha heshima zao kwa kufuata mfano wake wa kutumika, kufanikiwa na bila ya majivuno.
Taarifa ya familia iliwaambia wale washabiki wake: "ukitembea nje usiku ukaona mwezi unakuchekea, mfikirie Neil na umkonyeze."

NEIL ARMSTRONG - akichekiwa afya mwaka 1966 kwaajiri ya kuruka na chombo cha anga.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.