Asili Yetu © All rights reserved
DIANA KRALL
Diana mwanamuziki na mtaalamu wa kucheza na piano, juzi kati katika tamasha la Hollywood amemuenzi Neil Armstrong, (mtu wa kwanza kukanyaga mwezini) kwa kuimba wimbo wa "Fly Me to the Moon" wimbo ulioimbwa na mwanamuziki wa kijerumani "Heidi Bruhl" mwaka 1965.
Diana kwasasa yuko katika heka heka za kuandaa album yake inayofahamika kama "Glad Rag Doll". Mwanamuziki huyu atatumia vionjo vilivyotengenezwa tokea miaka ya 1920 na 30, ambapo wimbo mmoja katika album hiyo unaofahamika kama "Just Like a Butterfly That's Caught in the Rain" uliandikwa kwa mara ya kwanza miaka ya 1920 na kurekodiwa na "Annette Hanshaw mwaka 1927.
Mwanamuziki huyu wa miondoko ya Jazz "Diana Krall" alifunguka kuwa, kama wakati ungekuwa ukirudishwa nyuma, basi angechagua kuishi miaka ya 1920.
NEIL ARMSTRONG- binadamu wa kwanza kufika mwezini Julai, 20, 1969 amefariki dunia akiwa na miaka 82 (1930- 2012).
NEIL ARMSTRONG- binadamu wa kwanza kufika mwezini Julai, 20, 1969 amefariki dunia akiwa na miaka 82 (1930- 2012).


No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA