Header Ads

Breaking News
recent

MSEMO HATARI ULIOIBUKA KWA WATU - WENGI HULIA NA JAMBO HILI.

Nimekuwa nikifanya utafiti simple sana, kuhusiana na ahadi / promises au miadi ya  kibongo.

Niwazi kwamba kwa maisha ya sasa kila mtu ni researcher au mtafiti  mzuri katika maisha yake ya kila siku, endapo atakumbuka  kutofautisha jana na leo. Sikuwahi kulala bila kukumbuka yaliyonitokea mchana au niliyotenda kwa siku nzima na nitakayo tenda kwa siku inayofuata.
Pia sikuwahi kuamka asubuhi bila kufikilia nitafanya nini leo, ni wazi kuwa watu wengi hufanya maamuzi yao kabla na baada ya kuamka kitandani asubuhi. Maisha ya binadamu wa sasa yanategemea sana pesa hata kuliko kitu kingine kile, watu wanawaza usiku na mchana kupata riziki yao na pengine kusahau riziki halali hutoka wapi zaidi ya Muumba mbingu na nchi?

Naam, turudi kwenye point sasa, leo hii mtu akikwambia baadae au njoo baadae lazima kwanza uweke alama ya kuuliza, hivi ni kweli au? Baadae nyingi huwa ni njia za kushindwana na mtu katika miadi au maongezi, hivo mtu huona njia nzuri ya kumuondoa mtu katika maongezi au madai ni kumwambia njoo baadae! Huenda baadae yako ikawa ya ukweli lakini most of baadae si za ukweli.

Nimeshuhudia baadae nyingi zikisababisha dhuruma, ugomvi,machukizo, uhasama kwasababu wamechoka na baadae. Mimi sipingi slogan au neno sawa na baadae litumikalo na mtandao mmoja wa simu za mkononi hapa nchini, isipokuwa mbali na hapo watu wamekuwa wakilitumia vibaya neno hili kama kumpooza mtu anayehitaji huduma au msaada fulani, kwa mfano: maombi ya kazi, madeni, msaada nk. 

Baade hugeuka kuwa----- baadae sana...... kesho ..... wiki .....mwezi....miezi.....mwaka....miaka.......dhuruma........ugomvi......uhasama.......kifo / kilema / jela.

Tutimize jamani ahadi zetu au tuwe tu wakweli kwa mambo yasiyowezekana na sio baadae ya moja kwa moja.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.