Header Ads

Breaking News
recent

KAMPENI ZA UCHAGUZI MERU MASHARIKI ZA ANZA RASMI.

All rights reserved to Asili Yetu.

Mwenyekiti wa Chama Cha Maendeleo na Demokrasia 'Freeman Mbowe' akihutubia mamia ya wananchi wa Arumeru Mashariki waliojitokeza katika mkutano huo wa uzinduzi wa kampeni za CHADEMA.
Mh. Zitto Kabwe, Joseph Mbilinyi na mgombea ubunge Meru Mashariki, wakisalimiana na wananchi.
Hapa viongozi wa CHADEMA walikuwa wakiwasili mkutanoni.
 Katika mkutano huo, Mbowe alimtaka Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa kutoa tamko juu ya CCM kukiuka Sheria ya Uchaguzi kwa kutumia kiasi cha Sh220 milioni wakati wa mikutano miwili ya kupitisha mgombea wao wa ubunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki.

Mbowe alisema Sheria ya Uchaguzi mdogo imeweka kiwango cha juu cha matumizi ya fedha ambazo zinapaswa kutumika zisizidi Sh80 milioni.

“Tunamuomba Tendwa atoe tamko juu ya hili, kwani mkutano wa kwanza wa CCM walikuwa na wajumbe 1,034 ambao kila mmoja alilipwa posho ya Sh50,000 na walitumia zaidi ya Sh100 milioni na mkutano wa pili ulikuwa na wajumbe1,044 ambao walitumia zaidi ya Sh120 milioni,” alisema Mbowe.

Alisema chama hicho, kilikuwa na wajumbe 888 na kilitumia kiasi cha Sh6.2 milioni pekee kutokana na usafiri na chakula kwa wajumbe.

Akizungumzia uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Mbowe aliwataka wakazi wa jimbo hilo kutambua kuwa uchaguzi huo sio wa Meru pekee bali una sura ya kitaifa.

“Taifa zima linafuatilia Arumeru Mashariki kujua mnafanya nini, nawaomba sana mtuchagulie Joshua Nassari ili mtuongezee nguvu bungeni dhidi ya chama cha magamba kwani mbunge mmoja wa Chadema ni sawa na wabunge 30 wa CCM,” alisema Mbowe.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.