Header Ads

Breaking News
recent

NICKI MINAJI AZUA UTATA KATIKA TUZO ZA GRAMMY 2012.

All rights reserved by Victor Machota.

 Katika tuzo za Grammy 54 mwaka huu, ilikuwa na mbwembwe nyingi kufuatiwa mastaa wengi kukosa tuzo.Msanii Nicki Minaj aliingia stajini akiwa ametinga vazi lefu jekundu lenye picha ya kinyago, lakini hiyo haikuwashtua watazamaji saana bali mtu aliyekuwa ameambatana nae alionekana kuwa ni kiongozi wa kanisa katoriki, lakini alikuwa ni Papa bandia.

Kikubwa zaidi wakati Nicky akiingia stajini, video zilizoko nyuma ya staji zilikuwa zikionyesha kipande cha movie za kishetani, na hata wakati wakupafomu kuna mtu aliyekuwa kama kiongozi wa kanisa, akiongea kama mtumishi wa kanisani!!
Kitendo hicho kimewasikitisha sana waumini wa Kanisa Kathoriki, huku Academy record ya tuzo hizo za Grammy ikionyesha kutofurahishwa kwa kitendo hicho kwani hairuhusiwi kwa msanii yeyote kuingiza udini katika sehemu hiyo.Nicki Minaji hakupata tuzo yoyote zaidi ya kutumbuiza kimaajabu.


Huo ndio mpango mzima wa jinsi dunia inavyoenda, ni wazi kabisa kuwa tunakoelekea sasa kunatia wasi wasi, kama viongozi wa dini sasa wanaigizwa katika mambo ya kidunia, nafikiri sisi ambao hatujafika huko, basi tuwe macho na tushike imani zetu. Amen!

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.