Header Ads

Breaking News
recent

Utafiti: Faida za kuyatunza mayai ya uzazi ya binadamu kwenye barafu

Daktari Helen O'Neill, wa chuo kikuu cha London, anasema: " Ni bora kuondoa mwilini mwako na kuyatunza mayai yako ya uzazi mapema kuliko kusubiri." 

Lakini ni ''hakikisho kamili'' la kupata ujauzuito na wasichana wengi hawawezi kugaramia garama ya upasuaji na utanzaji wa mayai ya uzazi ambayo ni Euro -£5,000 kila mzunguko mmoja wa hedhi.

Daktari O'Neil anasema : "Faida za kuyatunza mayai ya uzazi kwenye barafu ni kwamba unachukua jukumu la kutumga mimba mikononi mwako.

 Kama ukifanyiwa uchunguzi na ikibainika kwamba una uwezo mdogo wa kutpata ujauzito ni vema kuchukua hatua mapema." 

Anasema kuna upungufu mkubwa wa mayai bora ya uzazibaada ya mwanamke kufikia miaka 30 - na kwamba ubora huo huendelea kupungua kadri miaka inavyokwenda. 

"Bahati mbaya watu wengi huanza kutunza mayai yao ya uzazi wakiwa na umri wa miaka 35, ambapo wanakuwa wamechelewa kidogo ," alielezea.

Nchini Uingereza, idadi ya wanawake wanaotunza mayai yao ya uzazi kwa ajili ya kupata watoto baadae imeongezeka kwa kiasi kikubwa.

Mwaka 2014, wanawake 816 walitunza mayai yao kwenye barafu kwa ajili ya uzazi wa baadae ilipanda na kufikia hadi asilimia 25% mwaka 2013, kulinga na takwimu za hivi karibuni kutoka mamlaka ya inayofuatilia masuala ya uzazi wa kusaidiwa nchini humo (HFEA). 

Hospitali ya wanawake ya London ya mtaa wa Harley, hivi karibuni iliripoti kuwa idadi ya wanawake wanaohudhuria kliniki zake za uzazi wa kusaidiwa fimeongezeka mara tatu kitika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

Kiwango cha uzazi wa kupozesha mayai kwenye friji kilikuwa ni sawa na 14% mwaka 2013, kulingana na mamlaka ya HFEA.

 Kiwango kilikuwa cha chini kwa wanawake wenye umri wa zaidi ya miaka 38.
Source: BBC Swahili

PAKUA NYIMBO ZILIZOTOKA WIKI HII>>>DOWNLOAD
SUBSCRIBE YouTube account yetu upate video zaidi.
Kupata Update kibao, like Facebook account yetu.
Twitter Account yetu>>>Asili Yetu Tanzania
 


No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.