Watu wengi wahofiwa kufariki katika shambulio huko Ras Vegas, Marekani
Stori zilizo enea hadi sasa ni kwamba, Mzee wa miaka 64 aliwafyatulia
risasi watu waliokuwa wakihudhuria tamasha la muziki na kuwaua watu takriban
zaidi ya 58.
Watu takriban 22,000 walikuwa wanahudhuria tamasha ya muziki wa country usiku wa Jumapili katika eneo la wazi karibu na uwanja mdogo wa ndege wa Las Vegas.
Milio ya kwanza ya risasi ilisikika mwendo wa saa nne usiku saa za Las Vegas (05:00 GMT).
Mshambuliaji aliwafyatulia watu risasi kutoka ghorofa ya 32 katika hoteli ya Mandalay Bay na baadaye akajiua kwa kujipiga risasi.
BBC
SUBSCRIBE YouTube account yetu upate video zaidi.