Header Ads

Breaking News
recent

Damian Marley afungunguka jinsi alivyofanya kazi na Jay Z katika wimbo wa 'Bam'

Stori zinatoka Jamaika kwa mkali wa Reggae Damian Marley baada ya kufanya kazi na mkali wa rap kutoka nchini Marekani, Jay Z katika wimbo wake wa 'Bam' ulioko katika Album yake mpya ya 4:44.

Damian  Marley katika mahojiano na Vlad tv ameelezea jinsi alivyorekodi wimbo wa "Bam" wa JAY-Z katika album ya 4:44 na the way walivyokuwa bega kwa bega na msanii huyo wakati wa kurekodi ngoma hiyo. 

Damian pia amedokeza kuwa JAY-Z alimtumia ndege binafsi ili imfuate Afrika na kumpeleka Jamaica kwaajili ya kushuti wimbo wake wa video. 

Alipoulizwa je, watu wa Jamaika walimchukuliaje Jay Z alipofika huko?, Damian alijibu>>> "ilikuwa ni kipande tu cha video alichokwenda kushuti 'scene', lakini kila mtu alimuonesha heshima".

Nusu nyingine ya mahojiano hayo, yalikuwa yanahusu album ya hivi karibuni ya Damian, 'Stony Hill', ambayo ameweza kuelezea kuhusu baba yake Bob Marley

Unaweza kuicheki video hiyo hapo chini>>>
  
SUBSCRIBE YouTube account yetu upate video zaidi

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.