Header Ads

Breaking News
recent

Baba yake Drake ajichora tattoo ya Drake katika mkono wake.

Drake msanii wa miondoko ya hip hop kutoka Canada na anayefanya shughuli zake za muziki nchini Marekani, amekuwa ni mtu ambaye amekuwa akionesha upendo kwa baba yake mzazi, Dennis Graham

Mara nyingi katika nyimbo za Drake amesikika akielezea jinsi baba yake ambaye pia ni msanii anavyo mtia moyo/inspire na kuhusu kwao  Memphis.
Dennis baba yake Drake ameonekana mara nyingi katika covers za muziki wa video ya Drake, kwa mfano cover art ya 6 God's More Life playlist.

 Haikuishia hapo Drake pia mwaka 2014 alionekana kuchora tattoo ndogo ya picha ya baba yake katika mkono wake, ambayo ilichorwa na mtaalam  Dr. Woo

Sasa safari hii bwana Dennis amelipa fadhira kwa mwanae Drake kwa kuchora tattoo ya uso wa Drake katika mkono wake wa kulia. Tattoo iliyochorwa na mchoraji wa tattoo Money Mike.

Baba yake Drake alitaka kuchora tattoo hiyo ili iendane na ile mwanae aliyoichora mkononi mwake mwaka 2014, na kuna tetesi kwamba, tattoo hiyo alichorwa bure na rafiki yeke huyo. 

SUBSCRIBE YouTube account yetu upate video zaidi

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.