Watu zaidi ya 200 wahofiwa kupoteza maisha katika tetemeko Mexico
Tetemeko baya la ardhi limekumba maeneo ya katikati mwa Mexico na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 200.
Tetemeko lenye nguvu ya kipimo cha saba nukta moja limedondosha karibu majengo 30 katika mji mkuu wa Mexico city.
Watu
wanaotoa huduma za dharura wakisaidiwa na mamia ya watu wanaojitolea
bado wanaendelea kutafuta manusura ambao wamefukiwa na kifusi.
Maafisa wa serikali nchini wanasema idadi ya waliokufa inaweza kuongezeka.
Mapema
mwezi huu tetemeko hilo la ardhi pia lilipita katika eneo la pani ya
kusini magharibi mwa Mexico na kusababisha vifo vya watu 90.
Stori na BBC


No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA