Header Ads

Breaking News
recent

Huyu ndio mwanamuziki aliyemtoa Tylor Swift namba moja ya iTunes UK

Baada ya msanii Tylor Swift kuteka mashabiki duniani alipoachia wimbo wake wa 'Look what You Made Me Do' na kushika chat za juu katika mtandao kama iTune, sasa ameweza kubwagwa na msanii mrembo kutoka Uingereza maarufu kama Megan McKenna.
 Megan McKenna, 24, ni msanii wa miondoko ya muziki wa Country pia anayefahamika katika uigizaji wa kwenye TV, inasemekana ndiye msanii aliyemnyang'anya nafasi ya kwanza katika chati za muziki za iTunes Uingereza.
Vitu 5 unavyopaswa kufahamu kuhusiana na mkali huyu Megan kutoka Ungereza aliyenyakua kiti cha Tylor Swift katika upande wa iTunes UK>>>
1. Megan alikuwa maarufu kupitia mashindano ya kuimba kupitia runinga. 

2. Megan hata hivyo umaarufu wake uliongezeka mara dufu pale alipoanza kuwa muigizaji mkuu katika maigizo kwenye TV.

3. Anafahamika pia kama mmiriki wa mgahawa alioufungua mwaka huu.

4. Kwa sasa Megan ameachia kazi zake mbili “High Heeled Shoes” na “Far Cry From Love” zilizoshika chati za juu iTunes Uingereza.

5. Megan anafahamika pia kwa kuwa na wafuasi wengi katika mitandao ya kijamii kama vile 616k Twitter na 2m Instagram.  

Endelea kufuatilia dondoo kibao za KITOFAUTI duniani kupitia blog yetu ya ASILI YETU TANZANIA. Pia subscribe You Tube account yetu  kupata update kibao. 

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.