China kuja na Treni yenye kasi zaidi ya Mwanga na Sauti, hii itapita Juu.
Kampuni ya Makandarasi kutoka China ya Aerospace Science and Industry
Corporation (CASIC), ipo mbioni kuanza ujenzi wa mradi wa treni za juu
(Flying Train) zitakazokuwa na kasi kubwa kuzidi ile ya mwanga na sauti.
Treni hizo ambazo zitakuwa zinasafiri kwenye bomba maalumu (vacuum tube) lililotegwa juu ya nguzo zitasafiri umbali wa kilometa 4000 kwa saa na kwa spidi hiyo zitakuwa ndio chombo cha kwanza cha usafiri kuwa na mwendo kasi zaidi duniani.
Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Liu Shiquan amesema bado wanafanya utafiti kuangalia ni jinsi gani mradi huo utafanikiwa ili kupunguza adha ya usafiri nchini china na nchi nyingine za bara la Asia.
“Tunaona dunia inakwenda kasi kwenye teknolojia watu wamechoka kutumia muda mwingi kwenye usafiri nadhani tunahitaji kufikiria zaidi kwani watu wanaongezeka na mahitaji yanaongezeka,“amesema Liu Shiquan kwenye mahojiano yake kwa lugha ya kichina na gazeti la The Paper.
Treni hizo ambazo zitaendeshwa kwa kutumia nguvu ya sumaku umeme zitaenda kwa kasi mara 10 ya treni za sasa ambazo zinaenda kasi zaidi duniani kwa kilometa 300 zilizozinduliwa mwaka huu nchini humo.

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA