Header Ads

Breaking News
recent

Angelina Jolie aonekana kukabiliana na matatizo ya kiafya.

Stori za mastaa zinagonga hodi hadi kwa staa wa nyota wa filamu duniani maarufu kama Angelina Jolie, katika mahojiano yake na chombo kimoja huko majuu, mkali huyu ameonekana kukabiliwa na matatizo mapya ya kiafya na kuonekana afya yake kuzorota kuliko kawaida.

Wakati akiipromote filamu yake mpya inayoitwa "First They Killed My Father", Angelina Jolie alifunguka kuhusi jinsi anavyokabiliana na hali ya baada ya kutarakiana na mpenzi wake Brad Pitt, 53,.

Angelina hakuishia hapo alidokeza kuwa amekuwa akikabiliwa  na matatizo ya kiafya kwa mwaka huu.

Na kufikia Aug. 25, alipotoka kuipa sapoti filamu yake mpya ndipo alipoonekana afya yake kuwa tofauti na siku za nyuma, kitendo kilichoibua maswali kwa watu wengi, je huenda ikawa ni baada ya kutarakiana na mpenzi wake Brad Pitt?.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.