Header Ads

Breaking News
recent

Sababu za kukosa usingizi ukiwa ugenini

Inawezekana wewe ni miongoni mwa watu ambao hukosa usingizi kabisa au kushindwa kulala vizuri pindi unapotembelea sehemu tofauti na uliyoizoea kama vile ugenini, hotelini na sehemu nyingine na unajiuliza ni kwa sababu ipi inakufanya uchelewe kulala au kutolala kabisa.
Sasa nimekutana na mtonyo huu ambao Wanasayansi wameelezea kuhusu kwa nini mtu hukosa usingizi au kutolala vizuri akiwa ugenini wakisema husababishwa na ubongo.
Mtu anapolala ugenini au mahala asipopazoea nusu ya ubongo wake ndiyo hulala lakini nusu nyingine inakuwa ‘active’ na hii ni kutokana na mabadiliko ya mazingira.
Fahamu kuwa jambo hili hupelekea mtu kuchelewa kupata usingizi na huwahi kuamka pengine isivyo kawaida na wakati mwingine awapo katikati ya usingizi huweza kushtuka anaposikia milio ya vitu kama ndege, mtu anatembea na vingine vingi.
Endelea kufuatilia dondoo kibao za KITOFAUTI duniani kupitia blog yetu ya ASILI YETU TANZANIA. Pia subscribe You Tube account yetu  kupata update kibao.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.