Teknolojia ya kuundwa kwa roboti zenye uwezo wa kuua yapingwa vikali.
Zaidi ya wataalamu 100 wa teknolojia
ya roboti wameutaka Umoja wa Mataifa kuchukua hatua ili kuzuia kundwa kwa roboti zinazoweza kuua.
Kwenye barua kwa Umoaj wa Mataifa,
wataalamu wa masuala ya teknolojia akiwemo tajiri Elon Musk, wameonya
kuwa, hatua hiyo itasababisha kuwepo kwa vita vitakavyohusisha roboti.
Wataalamu hao 116 wametaka kuwekwa marufuku ya kutumia teknolojia hiyo kuunda roboti inayoweza kutumiwa kama silaha.
Mwaka 2015 zaidi ya wataalamu 1,000 na watafiti waliandika barua wakionya kuhusua kuundwa kwa silaha kama hizo.
Kati
ya wale walioweka sahihi barua ya mwaka 2015 ni mwanasayansi Stephen
Hawking, na mwanzilishi mwenza wa kampuni ya Apple Steve Wozniak na
bwana Musk.
Roboti za kuua ni zipi?
Roboti
za kuua ni silaha ambazo zinaweza kuchagua na kuvamia kitu ambacho
zinakilenga bila ya kuelekezwa na binadamu. Tayari kwa sasa zipo lakini
kuboreshwa zaidi kwa teknolojia itachangia kuziwezesha kufanya hivyo.
Wale
wanaopendelea roboti hizo wanaamini kuwa sheria za sasa za vita
zinatosha kutatua shida yoyote ambayo itaibuka ikiwa zitatumiwa.
Lakini
wale wanaozipinga wanasema kwa roboti hizo ni tisho kwa binadamu na
teknolojia yoyote ya kuziwezesha kuuwa inastahili kupigwa marufuku.
Chanzo: BBC

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA