VITUKO: Mke aruhusiwa kumuacha mumewe, kisa nyumba yao haina choo cha ndani.
Mahakama kaskazini mwa India, imempa
ruhusa mwanamke katika jimbo la Rajasthan ruhusa aachwe na mumewe, kwa
sababu nyumba yao haina choo.
Jaji alisema kwenda kufanya haja nje ni kitu cha aibu, na ni kumuadhibu mwanamke, kukosa kumuweka mwanamke pahala salama anapokwenda haja.
Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF linasema kuwa karibu nusu ya watu nchini India, karibu watu milioni 600 hawana choo.
Mwaka uliopita mwanamke alikataa kuolewa na mwanamume mmoja katika jimbo la Uttar Pradesh baada ya mwanamume kukataa kujenga choo.
Na bbc
Endelea kufuatilia dondoo kibao za KITOFAUTI duniani kupitia blog yetu ya ASILI YETU TANZANIA. Pia subscribe You Tube account yetu kupata update kibao.

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA