Header Ads

Breaking News
recent

Floyd Mayweather amtwanga Conor McGregor na kuchukua ushindi, aongeza rekodi yake ya dunia ya 'mapambano 50' bila kupigwa

 Mchuano mkali wa ndondi kati ya Conor McGregor na mwanandondi Floyd Mayweather Jnr umemalizika huko Las Vegas, Nevada nchini Marekani, baada ya kuchelewa kuanza kwa muda wa saa moja hivi.

Floyd Mayweather Jnr ameibuka mshindi katika mchuano huo.
Maelfu ya watu walifika katika mji wa Las Vegas katika jimbo la Nevada nchini Marekani, kutizama mchuano huo mkali wa ndondi, unaofanyika leo Jumapili.
Masumbwi hayo yalikuwa ya raundi kumi. Awali wachanganuzi walisema kuwa Floyd Mayweather Jnr alikuwa ameanza kulemewa katika raundi tatu za mwanzo na mpinzani wake, kabla ya kujizoazoa na kuanza kumrushia makonde mazito mazito Conor McGregor, ambaye alionekana kulemewa hasa kuanzia raundi ya saba.
Alishindwa kuhimili makonde mazito ya Maywheather na kushindwa kumaliza raundi ya 10.

Lakini nyota huyo wa miaka 29, hawajawahi kushiriki mchuano wa makonde ya kulipwa- huku May-weather menye umri wa miaka 40 akitajwa kuwa mpinzani wake hatari zaidi katika masumbwi.

Endelea kufuatilia dondoo kibao za KITOFAUTI duniani kupitia blog yetu ya ASILI YETU TANZANIA. Pia subscribe You Tube account yetu  kupata update kibao. 

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.