Header Ads

Breaking News
recent

Floyd Mayweather afunguka baada ya Justin Bieber kumunfollow Instagram

Mkali wa masumbi na tajiri maarufu Floyd Mayweather Jr ametia neno baada ya hivi karibuni star wa muziki Justin Bieber kufanya maamuzi ya kum-unfollow katika ukurasa wake wa Instagram.

Mchongo wenyewe ulikuwa hivi, Aug 15 Justin Bieber, 23, alionekana kwenye video clip ya paparaz iliyomuonesha akitoa maoni yake kati ya mechi iliyopaniwa sana na mashabiki wa ndodi duniani ya Floyd Mayweather Jr., 40, na Conor McGregor, kuwa hadhani kama Floyd atamshinda McGregory.

Japo Bieber pia katika video hiyo hiyo alionekana akisema yeye bado yuko upande wa Mayweather

Japokuwa miezi ya hivi karibuni msanii huyo wa "Friends" ameamua kuwa mbali na Mayweather, uamuzi huwa wa Bieber umekuja baada ya kutoka kanisani.

Inasemekana kuwa alishawishika na mafundisho ya mchungaji ya kufuta matendo ya kale na kusafisha njia zake, ikiwa ni pamoja na kuondoa ushawishi mbaya katika maisha yake kama vile Floyd

Hivyo Justin alifika mbali hadi kum-unfollow Floyd! hii ni kwa mujibu wa chanzo -  TMZ

Kwa upande wa Floyd Mayweather amenukuliwa akisema “Anamlengo wa kanisa. Anamlengo wa timu mpya. Amejiweka kwa Mungu na kitu naweza kumpa ni ni heshima tu".  

Mayweathe aliongeza kuwa>>> "Siko hapa kuwa kinyume na kumzungumzia mtu yeyote vibaya. Kama sina kitu chanya cha kuzungumza, basi sitakuwa na chochote cha kuzungumza". 

Sababu ya mimi kuzungumza hivi: mtu niliye naye ugomvi ni Conor McGregor. Bifu yangu sio kwa mtu ambaye ni 'pop star'."

"Nampenda Justin Bieber na siku zote sitakuwa na chakumtakiza zaidi ya kumtakia mazuri zaidi”. 

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.