Ripoti kuhusu Simu za Note 7 zilizokuwa na tatizo la kuripuka yatolewa.
Uchunguzi uliofanywa na Samsung
kuhusu visa vya simu aina ya Galaxy Note 7 kushika moto, umebaini kwamba
visa hivyo vilitokana na kasoro kwenye betri.
Simu ambazo zilitolewa upya pia zilikuwa zinashika moto.
Lakini Jumatatu, Samsung imesema tatizo halikutokana na programu za simu hiyo iliyotarajiwa kutoa ushindani kwa simu za iPhone zinazotengenezwa na kampuni ya Apple.
Aidha, Samsung wamesema kasoro haikuwa kwenye sehemu
nyingine za simu hiyo ila kwenye betri pekee.
Hatua ya kuzichukua tena simu zote zilizokuwa zimeuzwa inakadiriwa kuigharimu kampuni hiyo ya Korea Kusini jumla ya $5.3bn (£4.3bn) na kuathiri pakubwa sifa za kampuni hiyo.
Kampuni hiyo imesema kasoro kwenye uchoraji wa muundo wa betri hizo pamoja na kasoro kwenye mfumo wa utengenezaji wa betri hizo, zilisababisha betri hizo ambazo ziliundwa na kampuni mbili kuwa na kasoro.
Kwa mujibu wa matokeo ya uchunguzi, matatizo yanatokana na betri hizo kuwa kubwa na hivyo kutotoshea vyema kwenye sehemu yake ndani ya simu.
Aidha, hakukuwa na nyenzo za kutosha za kukinga betri hizo dhidi ya joto.
Source: BBC Swahili
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA