Rais wa Marekani Donald Trump aondoa ufadhili kwa mashirika ya utoaji mimba
Rais wa Marekani Donald Trump ametia
saini agizo rasmi la rais kupiga marufuku kutolewa kwa pesa za serikali
ya Marekani kufadhili mashirika ya nchi za nje ambayo yanatekeleza au
kutoa habari kuhusu utoaji mimba.
Agizo hilo ambalo kirasmi linafahamika kama "the Mexico City Policy" (Sera ya Jiji la Mexico) huenda likayakera makundi ya kutetea uhuru wa wanawake kuamua kuhusu uzazi, ambayo tayari yametiwa wasiwasi na msimamo wake wa kupinga utoaji mimba.
Bw Trump anaunga mkono utoaji mimba upigwe marufuku Marekani.
Lakini hii si mara ya kwanza kwa marufuku dhidi ya ufadhili wa mashirika ya utoaji mimba nje ya Marekani kutolewa.
Rais wa Republican Ronald Reagan mara ya kwanza alianzisha Sera ya Jiji la Mexico mwaka 1984 na kuwa wa kwanza kupiga marufuku ufadhili huo.
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA