Helikopta ya kwanza ya abiria nchini China yenye uwezo wa kubeba tani 7 yaruka kwa mara ya kwanza.
Helikopta ya kwanza ya abiria nchini China imefanya safari yake ya
kwanza hii leo, ikiwa ni ishara ya maendeleo mapya katika sekta ya
usafiri wa helikopta nchini China.
Shirika la Usafiri wa Anga
nchini China limesema, helikopta hiyo AC352 inatumia injini mbili, ina
uwezo wa kubeba tani 7.5 wakati wa kupaa, na inaweza kubeba abiria 16.
Mbunifu mkuu wa helikopta hiyo Lu Weijian amesema, helikopta hiyo
inaweza kutumika katika usafirishaji wa pwani, uokoaji, utekelezaji
sheria, usafiri wa kawaida, na huduma za afya.
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA