Ripoti ya Shirika la Afya Duniani inasema, takribani watu zaidi ya milioni 1 wametibiwa homa ya Ini
Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) linasema zaidi ya watu milioni moja
katika nchi zenye kipato cha chini na cha kati wamepata tiba ya homa ya
ini aina ya C tangu kuanzishwa kwa tiba mpya miaka miwili iliyopita.
Katika
taarifa yake hii leo, WHO imesema wakati vijiua virusi vifanyavyo kazi
moja kwa moja (DAAs) vilipopitishwa kwa ajili ya homa hiyo mwaka 2013,
kulikuwa na hofu kuwa gharama kubwa itakuwa kikwazo cha kuwafikia watu
milioni 80 wenye homa ya ini sugu aina ya C.
Shirika hilo limesema licha ya mafanikio hayo kwa nchi kama vile
Misri, Morocco, Nigeria, Rwanda na Indonesia bado uhitaji ni mkubwa kwa
mamilioni ya wagonjwa duniani kote.
Kwa mujibu wa WHO, utashi wa kisiasa na uwakili wa asasi za kiraia ni
miongoni mwa sababu za mafaniko hayo dhidi ya homa ya ini aina ya C
ambayo kwa mwaka husababisha vifo vya watu takribani 700,000.
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA