Tajiri wa dunia Bill Gates aweka wazi mrithi wa mali zake.
![]() |
Bill Gate na familia yake. |
Bila shaka umeshawahi kufikiria kuhusu
mrithi wa mali zako siku ikitokea haupo duniani, japokuwa kwa tamaduni
za kiafrika ni watu wachache sana huwa wanaweka wazi au kuandika taarifa
kuhusu warithi wa mali zao pindi ikitokea wamefariki dunia.
Sasa leo nimeipata hii kuhusu atakayerithi mali au utajiri wa Bill Gates ambaye ni tajiri namba moja wa dunia kwasasa.
![]() |
Nyumba yake |
Kwa mujibu wake mwenyewe Gates amesema
hataacha utajiri wake unaotajwa kufikia Dola za Marekani Bilioni 81.7
kwa watoto wake watatu na badala yake atatoa kiasi dola za Marekani
Bilioni 70 kwa watu wanaohitaji msaada dunia nzima, na tayari watoto
wake wote wanajua kuhusu maamuzi yake na wamemuelewa.
kizungumza
kupitia kipindi cha Holly Willoughby na mtangazaji Ben Shephard,
Mmiliki huyo wa kampuni ya Microsoft mwenye miaka 60 amesema “Ndio,
watoto wetu wanapata elimu bora sana na tunawapa pesa za kutosha lakini
kuna siku watakwenda kuanza maisha yao na kufanya kazi zao.” – Bill
Gates
Bill Gates
amesema kuwa endapo ataruhusu watoto wake wawili wakike na mmoja wa wa
kiume warithi utajiri wake watakachokifanya ni kuzichezea tu pesa zake.
![]() |
Nyumba yake kwa ndani |
Mfanyabiashara huyo mkubwa amesema kuwa
ana uhakika watoto wake hawawezi kuwa masikini na ameshawawekea uhakika
wa maisha yao watakapoanza maisha yao siku za baadaye. Bill Gates na
mkewe Mellinda mwenye miaka 52 wana watoto watatu ambao Jennifer mwenye
miaka 20, Rory mwenye miaka 17, ana Phoebe mwenye miaka 14.
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA