Thursday, May 22 2025

Header Ads

TAMTHILIA YA "HER MOTHER'S DAUGHTER" EPISODE YA MWISHO.

 
Mio baada ya kuona maji yamemfika shingoni, anaamua kufanya unyama, huku akiuungana na mwanae Diego, ili kuwakomoa Lucas pamoja na familia ya Theresa.

Julio baada ya kuhofia kuwa familia yake inaweza kufanyiwa unyama na Mio, sasa anaamua kuihamisha familia yake na ya Theresa, lakini Theresa anaonekana kutokubali yeye kuondoka nao, kwani alidhani Diego ambaye alikuwa ni mtoto wake aliyetoroshwa na baba yake Mio na kuishi nae kwa miaka mingi, kuwa huenda angebadilika na kumkubali.

Lucas akiwa anazungumza na mke wake Yolanda, mara Yolanda alimtaarifu Lucas kuwa wanajiandaa kuondoka, lakini kumbe Mio alikuwa kajibanza sehemu na kusikiliza taarifa hizo, hivyo alipanga jinsi ya kwenda kuwateka akina Theresa kabla hawajaondoka.

Theresa akiwa katika harakati za maandalizi ya safari nyumbani kwa Beatrice, mara Margaux aliamua kutoka nje na kuelekea katika gari zao walizokuwa tayari wamekwisha andaa, lakini kufika kule alikutana na miili ya maskali waliouwawa na kuwekwa katika buti ya gari.

Akiwa bado anashangaa shangaa, mara Mio alitokea kwa nyuma na kumteka na kumuonya kuwa akipiga kelele angempiga risasi. Mio aliamua kumpigia simu Theresa na kumpatia masharti kuwa asipokuja hapo, atamuuo mwanae Margaux. Theresa ilibidi aje na kuungana na Margaux, wote wakiwa mateka.

Baada ya muda Beatrice na Celyn nao walijitokeza, nao walitekwa na kuingizwa katika gari moja na kutimua mbio pasipojulikana. Wakati huo Ethan aliwasili na kufanikiwa kumpigia simu Liam na Julio pia.

Walifanikiwa kuwafuatilia akina Mio na Diego, lakini wakiwa njiani, Mio alitoa bastola na kuwalenga, ambapo risasi zilifanikiwa kuharibu matari ya gari ya Julio na Liam, lakini Ethan aliwasili na gari lake na kuwachukuwa, japo walichelewa kidogo lakini walifika walipowateka akina Celyn na kuzuiliwa na maaskari.

Mio alimuamlisha Diego alipize kisasi kwa kumlipua risasi mama yake yani Theresa, lakini Diego kwa uchungu aliamua kupiga risasi juu, kitu ambacho kiliwashtua maaskari nje na kuamua kuzama ndani.

Mio kuona Diego ameshindwa kumlipua Theresa, aliamua kumnyang'anya bastola, lakini wakati wakivutana vutana, risasi iliponyoka na kumfyatua Diego na kuanguka chini. Mio alipigwa na butwaa na kuishiwa nguvu na kukaa chini. Theresa akiwa anamwaga machozi aliinua ile bastola na kumlenga Mio mkononi na kukimbia.

Mio aliamka na na kuwasaka kina Theresa, alifanikiwa kuwapata na kutaka kuanzakuwauwa, mara Julio alitokea kwa nyuma na kumpiga risasi Mio, alianguka chini japo hakuachia bastola yake. Liam na Ethan tayari waliwasili hapo. Wakiwa wote wanakumbatiana, mara Mio aliinuka na kumpiga risasi Theresa mgongoni, lakini pia maaskari pia walikuwa wamekwisha wasili na kummwagia risasi zaidi ya sita mgongoni na kufariki hapo hapo.

Theresa alikimbizwa hospitali, huku Lucas akitupwa jela japo Yolanda mke wake alimtembelea huko na kuombwa msamaha, wote walifurahi na kusameheana. Ethan na Margaux walioana, huku Liam na Celyn nao wakifanya vivyo hivyo.

Margaux na Celyn wote walikuwa wajawazito na kujifungua watoto, mara familia nzima ya Liam na mama yake Ethan walionekana kwa pamoja huku familia nzima ya Theresa na Theresa mwenyewe kwani alikuwa tayari kapona pamoja na Beatrice na watoto wa Celyn na Margaux walionekana wote wakifurahia, na hadi kufikia hapo Tamthilia ya "Her Mother's Daughter" ilifikia mwisho.

'''''''''''MWISHO'''''''''''''''

Karibu katika dondoo nyingine za Tamthilia mpya ya "Be Careful with My Heart" hapa hapa Asili Yetu Tanzania.

Leave a Comment

Powered by Blogger.