TAMTHILIA YA "HER MOTHER'S DAUGHTER (Episode ya 69) MAUWAJI YAPANGWA KUTOKEA, HUKU PENZI LA CELYN NA LIAM LIKIPANUKA.
![]() |
Aliyeigiza kama "Diego" |
Ukweli ni kwamba, yule jambazi ambaye ni baba mzazi wa Diego (Joshua) alitumwa na Lucas kumuadabisha Theresa, lakini yeye kwasababu alikuwa na kinyongo na Lucas cha wakati akiwa jela Lucas hakumsaidia kutoka mapema, hivyo aliamua kumpiga risasi Julio ili kumkomoa Lucas.
Lucas alipojaribu kumkaripia kwakuvunja taratibu zao, jambazi alikuja juu na kuanza kugombezana na Lucas, japo Lucas alisema hawezi kumtisha kwasababu anapesa na nguvu (power). Lakini katika baadhi ya mazungumzo yao, kumbe Beatrice alikuwa akimsikia baba yake yani Lucas alivyokuwa akibishana mara kwa mara na jambazi.
Kumbuka jambazi aliwahi kuwa mpenzi wa Theresa kipindi cha nyuma, hivyo mtoto wa jambazi ambaye alilelewa na Theresa alikuwa ni Diego wakati huo aliitwa Joshua, kabla ya baba yake kumchukua kwa nguvu na kumjaza maneno Diego kuwa mama yake alimterekeza na ndiye aliyemsababishia matatizo katika maisha.
Jambazi alinyemelea nyumbani kwa Theresa mida ya usiku, wakati huo Theresa alitoka nje kutupa taka taka, alimuona Jambazi amesimama pembeni ya mti, huku akiwa amejifunika kofia ya mduara uliofunika hadi macho. Theresa alimuita jina lake na kumfuta, waliteta pale na Theresa kumtupia maneno kadhaa.
Jambazi alimrukia na kumkamata Theresa kama vile kumng'ang'ania, alipiga kerere, jambazi alimwambia, "nitaripiza kisasi kwa kuuwa familia yako mtu mmoja baada ya mwingine, na huenda wamwisho watakuwa ni mapacha wako" yani Margaux na Celyn.
Beatrice aliamua kumfuatilia baba yake nyuma, kumbe alikuwa akienda kuongea na jambazi, wakati wakiwa wanasutana na jambazi, Beatrice alishuka ndani ya gari na kuwafuata. Alipofika alikuta sura ile ile inayotafutwa na polisi kwa tuhuma za kumpiga risasi mume wake. Beatrice bila kujali alimrukia na kumsukuma hadi chini.
Lakini baba yake alimzuia na kumwambia amuache kwani huyo jambazi anasiri nyingi sana zinazomuhusu yeye na kampuni yake, kwani akikamatwa baba yake naye anaweza kufungwa jela na kufirisiwa kabisa. Beatrice hakuamini kile alichokisikia kutoka kwa baba yake, aliondoka kwa hasira huku baba yake akimpigia magoti ili asamehewe, lakini Beatrice alikataaa kata kata.
Jumbani kwao Margaux, anawaona Celyn na Liam wakiwa bize wakizungumza, alishawishika kusogea na kusikia walikuwa wakizungumzia nini. Ile Margaux anafika tu alikuta Liam akimuuliza swali adimu sana "unakubali kuolewa na mimi?" Celyn alicheka kwa furaha na kusema "ndiyo". Kwa bahati nzuri Ethan alikuwa kajibanza pembeni, wote Ethan na Margaux walisikia swali na jibu.
Ethan alimfuta Margaux na kumuuliza umesikia mazungumzo hayo?
DONDOO ZIJAZO:
Je Ethan ataitumia nafasi hiyo kumtia Margaux katika himaya yake ya penzi? Je ulinzi wa Lucas dhidi ya jambazi utafanikiwa? Theresa hana ulinzi wowote na alitishiwa na jambazi, je familia yake itasalimika? Diego ameonekana akimuokoa Celyn alikotekwa na jambazi na Celyn amemtambua kuwa Diego ndiye Joshua kaka yake, je nini kitaendelea? Karibu Asili Yetu Tanzania kwa dondoo kibao... LIKE PAGE YETU HAPA UPATE HABARI KEM KEM...Bofya hapa https://www.facebook.com/pages/Asili-YETU-Tanzania/193268684090826
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA