Header Ads

Breaking News
recent

TAMTHILIA YA "HER MOTHER'S DAUGHTER" (Episode ya 56) SIRI YAFICHUKA "MARGAUX" AFAHAMU KUWA NI PACHA WA "CELYN".

Kutoka kushoto ni Liam, Celyn,Margaux na Ethan
Katika sintofahamu iliyochukua kipindi kirefu baada ya siri nzito za wazazi wa wasichana walioishi katika maisha ya kutoelewana kwa kipindi kirefu, sasa mambo yawekwa wazi baada ya harakati kibao kufanyika.

Margaux amemkubali Ethan amsaidie kuwatafuta wazazi wake, kwasababu hakuwa na chaguo lolote isipokuwa tu kumkubalia Ethan ili aweze kufanikisha kuwapata wazazi wake.

Siku iliyofuata Ethan anampitia Margaux kwao na kuamua kwenda katika kile kijiji kunakosemekana kuwa yule bibi aliyemzalisha mama yake na Margaux yupo. Wakiwa katika harakati za kumtafuta huyo nesi, mara Zacharis na Oscar wanawaona Margaux na Ethan, ghafla wanajificha na kushikwa na hofu.

Zacharis na Oscar wameshikwa na hofu baada ya kusikia harakati za kutaka kujua ukweli wa wazazi wa Margaux, hivyo wanapanga mbinu za kuutoa ukweli huo, lakini babu yake Celyn yani Zacharis anaamua kumfuta Margaux kwao, akiwa anaongea nae mara babu yake Margaux anatokea na kumkaripia sana Zacharis.

Celyn aliporejea Margaux akamwambia kuwa amzuie babu yake kuwa anakuja hapo, lakini Celyn anakataa na kusema kuwa anahaki ya kuja kumsalimia kwasababu yeye ni familia pia. Teresa anapata habari kuwa baba yake alikwenda kwa akina Margaux na kufanyiwa fujo. Teresa anafunga safari kwa hasira na kwenda hadi kwa Beatrice na kumwambia chochote kitakachotokea kwa baba yake hivyo wajitayarishe kumkabili, kwasababu anaugonjwa wa moyo.

Liam na Celyn bado mambo si mazuri saana lakini Celyn anaonekana kuanza kulainika, yani kuanza kuwa na wivu na Liam tena.
Ethan anaonekana kumpa ushirikiano Margaux, lengo likiwa moja tuu, arudishe penzi la Margaux kwake, na safari hii katika hali isiyokuwa ya kwaida, Margaux na Ethan wanafanikiwa kumpata yule mkunga aliyekuwa na siri kuhusu watoto wa Teresa.

Margaux anakuja nyumbani huku akionyesha hali ya mshangao hadi kwa mama yake na kumwambia "mama mama, nimempata yule nesi, kumbe mjomba Oscar ndiye aliyekupatia mtoto ambaye ndio mimi na kumbe pia mimi na Celyn ni mapacha". Wote walibaki midomo wazi. Huko nako Zacharis anatoboa siri kwa bibi yake na Celyn na kumwambia kuwa Margaux na Celyn ni mapacha.

Dondoo zijazo; Je nini kitatokea baada ya Margaux kujua ukweli kuwa Celyn ni pacha wake wa mama mmoja yani Teresa? Je yule aliyoko jela ni nani na anampango gani? Teresa je atamtaka Margaux arudi nyumbani kwao? Na je Margaux atamkubali Teresa kama mama yake mzazi? Fuatilia dondoo zijazo hapa hapa ASILI YETU TANZANIA.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.