AsiliYetuTz: REBECCA MALOPE MUIMBAJI MAARUFU WA NYIMBO ZA INJILI AFRIKA KUSINI.
Muimbaji wa nyimbo za Injili nchini Afrika ya Kusini, maarufu kama Rebecca Malope, alizaliwa mnamo mwaka 1968. Historia ya mwanamuziki huyu wa nyimbo za Injili, ambaye alijipatia jina pia kama "Malikia wa nyimbo za Injili Afrika", ilianzia mwaka 1986 alipokuwa na miaka 18 tu, ndipo alipoamua kuondoka kwao akiwa na dada yake Cynthia na ambapo mwishowe walitamatia katika mji wa Johannesburg huko huko Afrika ya kusini.
Safari hiyo ya msanii huyu wa Nyimbo za Injili, ilikuja kuzaa matunda yanayozidi kukonga nyoyo za mamilioni ya watu duniani. Rebeka pia ni mtangazaji wa kipindi cha luninga kiitwacho "It's Gospel Time" kinachohusu Injili.
Ndani ya takribani mika 27 katika kazi yake ya muziki, Rebecca amekwisha toa album za muziki wa Injili takribani 32. Pia anatuzo za muziki zaidi ya 29. Huyu ndiye Rebecca Malope ninayemzungumzia leo, msikilize ladha yake hapo chini.

.jpg)

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA